Wednesday, December 8, 2010

......wakati kuna uhaba wa kondomu...

Ni hivi juzi tukiadhimisha siku ya ukimwi ulimwenguni na hapa nchini wito wa kuimarisha vita dhidi ya HIV ulitolewa na wadau mbalimbali. lakini la kusikitisha kuwa ni kwamba huenda tukakosa kukabiliana na maradhi haya, huku ikihofiwa kuwa viwango vya maambukizi hayo viko juu zaidi hapa nchini. Hata hivyo kama alivyosema papa benedict wa 16 kwamba wakati mwengine ngono haizuhiki, inahitaji kutumia kinga kujizuia na maradhi ya ukimwi na magonjwa mengine ya zinaa. Inasemekana kwamba maeneo mengi hapa nchini yanakabiliwa na uhaba wa mipira ya kondomu licha ya serikali kuagiza mipira bilioni 41 miezi miwili iliyopita. Hivi inamaanisha takribani watu bilioni 41 walishiriki ngono miezi hiyo miwili?? ni wazo tu. kwa kawaida Desemba ina bashasha mingi sana..kwanza masuala ya tohara ambayo yanashirikisha watu wa tabaka mbalimbali wanaokutana bila kufahamiana..hapa kuna uwezekano wa mahusiano ya mapenzi kimwili, krismasi vile vile hii hapa inanukia, lakini la kusikitisha ni kwamba huenda tukalazimika kusubiri kwa muda kabla ya mipira ya CD kufika nchini. huku niliko kuna uhaba.. I say imekuwa vigumu kupata mipira hii, kwa chemist, shop na maeneo mengine hapa niliko..kiu nayo haina huruma. inabidi tuzuie. wakati huu tafadhali tujizuie na ngono ya kiholelea hadi kinga itakapoletwa kwetu.

No comments:

Post a Comment