Tuesday, December 7, 2010

Eti Kalonzo atapenya katikati yao!

Makamu wa rais Kalonzo Musyoka, anaendelea kushtumiwa, kuhusiana na matamshi aliyotoa mwishoni mwa juma, kwamba viongozi walioitisha maandamano ya umma kulalamikia matokeo ya uchaguzi uliozua utata hapa nchini,ndio wanafaa kushtakiwa. waziri wa ustawi wa mikoa Fred Gumo, sasa anadai Kalonzo ni mjanja na kwamba ana mpango wa kunufaika kisiasa kutokana na suala la mahakama ya ICC ambalo limesababisha tofauti za kisiasa kati ya baadhi ya viongozi. Gumo anadai kuwa kalonzo ana njama ya kupita katikati ya viongonzi wawili ambao anatarajia kubuni muungano na wao.
Ni juzi ambapo kalonzo alinukuliwa akimshtumu Waziri mkuu raila odinga na kutanganza kumuunga mkono mbunge William Ruto. Aidha alisema kuwa wataendelea kushirikiana na naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta kubuni muungano utakao wawezesha kukabiliana na mahasimu wao kisiasa. Hata hivyo inaonekana kana kwamba ujanja wa kalonzo umeonekana wazi baada ya wanasiasa kadhaa kusema kuwa anatumia fursa ya tetesi inayozingira viongonzi hao wawili kwamba huenda wakaenda hague mwakani kujinufaisha katika kujitafutia uungwaji mkono katika maeneo anayowakilisha. Gumo hata hivyo alishangaa kwamba viongozi waliopinga mpango wa kubuniwa kwa mahakama maalum ya hapa nchini kuwashughulikia washukiwa wa ghasia, sasa ndio katika msitari wa mbele kupinga uchunguzi wa mahakama ya ICC.

No comments:

Post a Comment