Thursday, December 9, 2010

Kwa nini Kenya hatuwezi kuzalisha ARV

Taarifa za hivi punde kuwa huenda mataifa ya Bara ulaya yakaingia katika mikataba na India katika kuzalisha dawa za kupungunza makali ya HIV ni kero kubwa na habari za kusikitisha kwa bara Afrika na Kenya kwa jumla. Ina maana kwamba huenda mataifa yanayotegemea dawa hizi kutoka nje, zikalazimika kuongenza gharama yake. Kwetu hapa Kenya, waathiriwa wa ugonjwa wa ukimwi wamekuwa wakipokea tembe hizo kwa bei ya chini lakini hali hii huenda ikabadilika kufuatia uamuzi wa hapo kesho. India ni moja wapo ya mataifa ambayo yanazalisha kiwango cha juu cha dawa hizo na endapo itatia sahini mikataba na mataifa ya bara ulaya ina maana kwamba uwezekano wa kupatikana kwa dawa hizo huenda ukaathirika. Monique Tondo ni afisa wa afya kutoka shirika la madakatari wasiokuwa na mipaka ya watu wanaoishi na virusi vya HIV yanayotegemea kuwepo kwa ARV na anasema kuwa huenda mkataba huo ukazidisha gharama ya ARV. Hii ni changamoto kwa mataifa ya bara Afrika kutafakari mbinu za kuzalisha dawa hizi ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya HIV. Hakika mnyongee hana haki, lakini tusizoee kukubali hali hii ya unyonge...sisi pia tuna uwezo. Ebo! jioni poa

No comments:

Post a Comment