Wednesday, December 1, 2010

ama Kweli eLImu maanake nini....?

Leo napenda tulitupie macho suala zima la elimu ambalo naamini ni sehemu kubwa ya maisha. Hii inatokana na ukweli kwamba kama hatutakuwa katika utafutaji wa elimu hii kama wanafunzi, basi tuko katika matumizi yake baada ya kuwa tumeichuma katika nyakati mbalimbali na viwango mbalimbali. Hata hivyo ukweli unabaki kuwa elimu haina mwisho. Wadau, nimetafakari kiundani kuhusu nini hasa maana ya elimu, baada ya kusoma ni wengi ambao wanaanza kuwaza na kuwazua na kuwazua jinsi watakavyoweza kujinufaisha na kisomo chao, lakini kuna wengine ambao wanageuza elimu kuwa chanzo cha kuchakachua na kuharibu msingi za maisha bora ya kijamii.Ni watu wa aina hii ndio ningependa waelewe kwamba: Elimu ni muhimu katika kusaidia kupambana na mazingira yetu, ili hatimaye, tuweze kuwa na mahali pazuri zaidi pa kuishi. Elimu inapaswa kutusaidia kuona uhalisia wa maisha ya kawaida, kwa kujenga maadili na utu wema....ni wazo tu wadau..siku poa!

No comments:

Post a Comment