Kundi la National Emerging youth for change linamtaka balozi wa marekani nchini Kenya, Michael Ranneberger kukoma kushiriki siasa za kisiri na badala yake kutangaza msimamo wake na nia yake ya kisiasa. Kundi hilo limemtaka balozi huyo kukoma kutoa ufadhili wa kifedha kwa baadhi ya makundi na jamii fulani. Mwenyekiti wa kundi hilo Daniel Mwangi amesema kuwa iwapo Ranneberger hatofanya hivyo kwa muda wa saa 48 basi kundi lake litaongoza maandamano ya vijana wote katika taifa hili kupinga balozi huyo. Ni hivi juzi msemaji wa serikali Alfred Mutua alisema kuwa kuna serikali za kigeni ambazo zinafadhili vijana kwa njama ya kunyakua uongozi wa taifa hili huku waziri mkuu Raila Odinga pia akikashifu hatua ya mabalozi kufanya ziara za kisiasa. Madai ya Mutua yalipuziliwa mbali na Marekani, ambao walisisitiza wanafadhili makundi ya kuratibu maendeleo na wala sio ya kuzua vurugu au kuipindua serikali ya muungano.
No comments:
Post a Comment