Wednesday, February 2, 2011

EDUCATION TASK FORCE LAUNCH////////MUDAKI


WIZARA YA ELIMU IMEZINDUA RASMI JOPO KAZI LA KUANGANZIA NA KURATIBU MABADILIKO KATIKA SEKTA YA ELIMU KUAMBATANA NA KATIBA MPYA. NA KAMA ANAVYOARIFU NEWTON MUDAKI, JOPOKAZI HILO LINA MUDA WA MIEZI SITA KUKAMILISHA JUKUMU HILO KABLA YA KUWASILISHA MAPENDEKEZO YAKE BUNGENI ILI KUIDHINISHWA.

AKIZINDUA RASMI JOPO KAZI HILO, WAZIRI WA ELIMU PROF SAM ONGERI AMESEMA IPO HAJA YA KURATIBU MABADILIKO YA KINA KATIKA SEKTA HIYO KUHAKIKISHA UGAVI SAWA WA RASLIMALI NA VILE VILE KUIMARISHA VIWANGO VYA ELIMU NCHINI. AIDHA JOPO HILO LINATARAJIWA KUFANYA UCHUNGUNZI KATIKA SEKTA HIYO KUTATHMINI UDHAIFU NA UWEZO WAKE.WAKATI HUO HUO WAZIRI ONGERI AMEWATAHADHARISHA WAKUU WA SHULE DHIDI YA KUWALAZIMISHA WANAFUNZI KURUDIA MADARASA. AMEWATAKA KUTUMIA MBINU MBADALA KUTOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WANAOPITIA WAKATI MGUMU SHULENI.

AIDHA WAZIRI ONGERI AMETETEA MPANGO WA SERIKALI KUZIPANDISHA HADHI SHULE ZA UPILI ZA MIKOA HADI KUWA ZA KITAIFA KATIKA KAUNTI ZOTE. ONGERI AMEPUZILIA MBALI TETESI ZINAZOTOLEWA NA WATAALAM WA MASUALA YA ELIMU KUWA HUENDA HATUA HIYO IKAATHIRI VIWANGO VYA ELIMU NCHINI NA KUSEMA KUWA WANALENGA KUONGEZA IDADI YA WANAFUNZI WANAOJIUNGA NA SHULE ZA UPILI.KULINGANA NA ONGERI KUPANDISHWA HADHI SHULE HIZO NI NJIA MOJA YA KUHAKIKISHA KATIBA INATEKELEZWA KWA KUANGAZIA USAWA KWA WOTE WAKATI WA KUGAWA RASLIMALI ZA KITAIFA.

PNU TO WITHDRAW FROM COALITION//////MUDAKI


chama cha pnu kimetisha kujiondoa kutoka serikali ya muungano kutokana na mzozo unaoshuhudiwa kwa sasa.wakizungumza na wanahabari wabunge wa chama hicho wanasema kuwa hatua ya rais mwai kibaki kuwateua wakuu katika idara ya mahakama ndio sababu kuu ya kushuhudiwa migawanyiko serikalini hali inayowafanya kuchukua hatua hiyo ya kujiondoa.newton mudaki na mengi zaidi.

WABUNGE HAO aidha WANATAKA KUANDALIA KWA MKUTANO WA KITAIFA WA WAJUMBE WA CHAMA HICHO KATIKA MUDA WA SIKU ISHIRINI NA MOJA  ILI KUJADILI  IWAPO CHAMA HICHO KITAJIONDOA KUTOKA SERIKALI YA MUUNGANO AU LA.KIONI ANASEMA KUWA MGOGORO UNAOENDELEA KATIKA SERIKALI YA MUUNGANO HAUFAI KWANI VIONGONZI WANAJITAKIA MAKUU HUKU WAKISAHAU KIINI CHA KUBUNIWA KWAKE.
KUHUSU UTEUZI WA  WAKUU WA MAHAKAMA ULIOFANYWA NA RAIS MWAI KIBAKI HIVI MAAJUZI, VIONGOZI HAO WAMESISITIZA KUMUUNGA MKONO RAIS KIBAKI HUKU WAKIMTAKA WAZIRI MKUU RAILA ODINGA KUWAOMBA RADHI WAKENYA BAADA YAKE KUKIRI KUSHAURIANA NA RAIS. KWA UPANDE WAKE NAIBU MWENYEKITI WA CHAMA HICHO JAMLECK KAMAU AIDHA AMEISHTUMU TUME YA MAGEUZI KATIKA IDARA YA MAHAKAMA (JSC) KWA KUPINGA UTEUZI HUO. MBUNGE HUYO WA KIGUMO AMESEMA KUWA TUME HIYO HAINA HAKI YA KUFANYA HIVYO KABLA YAKE kupigwa msasA.