Saturday, January 15, 2011

Wakati Rais anamezea mate..'mawezere'

Nimeipata hii picha na ikanifurahisha sana. eti kwamba Rais Obama anaipa kijicho "manyuma" ya huyo dada.....
Nilipata hii comment kwenye hii picha: "Honestly... i think sarkozy ndio alikuwa ana introduce obama to tht kind of life his known for dating models en kwani wats the harm in checking out fyn ass. Obama kip it going theas stil mo to come."
 

Thursday, January 13, 2011

Tahadhari......Matapeli wanaojifanya maafisa wa jeshi

Wizara ya ulinzi sasaimetoa tahadhari kwa umma dhidi ya genge moja la matapeli, ambalo limekuwa likiwatoza wananchi pesa kwa ahadi za nafasi za kazi ya jeshi. Kundi hilo limekuwa likidai wana uhusiano wa karibu na maafisa wa ngazi za juu katika idara ya ulinzi.

Jamaa hao wamekuwa wakitumia Mpesa zilizo na majina ya maafisa hao wa kijeshi hususan kuwahadaa wananchi kwa vile unapotuma pesa, majina ya maafisa wa kijeshi ndiyo hujiandiklisha, na hivyo kutoa dhana kwa mwananchi asiye na fahamu kuwa pesa zake zimefikia maafisa hao wa kijeshi.

wizara ya ulinzi hivyo inawatahadharisha wakenya kutohadaiwa na mtandao huu wa matapeli,kwa vile nafasi za kazi katika idara ya jeshi hutangazwa wazi magazetini.

Thursday, January 6, 2011

Gender affairs.....

Women barred from attending a meeting organised by DPM Uhuru Kenyatta:

Ni mkutano unaokisiwa kujadili uridhi wa uongonzi wa nchi baada ya kustaafu kwa rais Mwai kibaki. Duru zinaarifu kuwa wajumbe na wafanyibiashara wanaotokea mkoa wa kati walijadili nani kati yao atapeperusha bendera ya urais kutoka eneo hilo, should Uhuru be stopped from running the presidency by the Hague related issues. Itakumbukwa uhuru ni kati ya washukiwa sita wa ghasia za baada ya uchaguzi.

Swali kuu hata hivyo ilikuwa, Ni kwa nini wanawake na vyombo vya habari, bila kujali jinsia, walifungiwa nje ya mkutano huo? taarifa zaidi soma hapa

Maua ya plastiki yapigwa marufuku

Shirika la mazingira nchini NEMA limepiga marufuku matumizi ya 
maua ya plastiki na baadhi ya makaratasi mepesi ya plastiki. kaimu 
mkurugenzi wa shirika hilo Ayub Macharia tayari ametoa muda wa 
miezi tatu kwa shirika la kukadiria ubora wa bidhaa KEBS kutimiza 
marufuku hiyo. wale watakiuka sheria hiyo watachukuliwa hatua kali 
za kisheria.

Saturday, January 1, 2011

Happy 2011 - Breakthrough Unlimited

Leo januari Mosi mwaka wa 2011 iwe mwanzo wa kheri, baraka na fanaka kwako msomaji wa blog hii.
Naomba kwamba kurunzi ya mema ikumulike daima leo na milele, wewe na familia yako (yenu) na marafiki wote.
Ndio mwaka wa vitendo kwangu wakati najitoa kushughulikia wasomaji wa blogu hii kwa taarifa tendeti na umbeya wa mtaa kwa mtaa.
Mimi Newton nawatakieni mwaka mpya wa 2011, wenye fanaka na uwezo. Soma Isaiah 60:22.

Heri ni malize hivi: Gbogbo aye ewa bami gbe ga!

HAPPY 2011.................................*****