Thursday, December 9, 2010

Human Rights Day.....

Wakati Kenya inajiunga na ulimwengu katika kuadhimisha siku ya haki za binadamu hapo kesho, ni dhahiri kuwa Kenya tumepiga hatua katika kupigania haki za binadamu. kupitishwa kwa katiba mpya ni dhihirisho tosha kuwa wakenya wako tayari kutetea haki zao kwani vipengee vingi katika katiba hiyo vinazingatia haki za binadamu. hakuna njia nyingine ambayo Kenya tungepata haki zetu bila sheria thabiti za kuzingatia haki za binadamu nchini isipokuwa kwa kupitishwa kwa katiba hiyo. hata hivyo tatizo kubwa ambalo taifa hili linafaa kujiondoa kabisa ni  kubaguana kikabila ili kuhakikisha kuwa kila mkenya amepata haki sawa katika kila nyanja huku tukinyoshea kidole cha lawama viongozi serikalini kwa kuendeleza uovu huo. Wakenya tusimame tupigane na ubaguzi.

No comments:

Post a Comment