Saturday, December 11, 2010

Jamhuri Day....miaka 47 sasa

Wakenya hapo Kesho tunaadhimisha makala ya 47 ya sherehe za Jamhuri. Itakuwa ni siku ya kipekee ikizingatiwa kuwa hii ni adhimisho la kwanza chini ya katiba mpya. Mbali ya ile feeling ya sherehe, lazima tujiulize tunajivunia nini miaka hii yote. Rais Mwai Kibaki na Waziri mKuu Raila Odinga wataongonza sherehe hizo katika uwanja wa Nyayo. Linalonikera ni kwamba wakati tukiadhimisha Jamhuri day ni kuwa shughuli ya utekelezaji wa katiba kufikia sasa imekwama kutokana na mzozo wa maeneo bunge. Sio haki kwa wanasiasa kusimamisha shughuli ya utekelezaji wa katiba kwa sababu ya matakwa yao ya kibinafsi, wanapaswa kutekeleza majukumu tuliyowapa. Naomba kwamba katiba hotuba zao, viongonzi hao wawili watawashurutisha wabunge kuzika tofauti zao na kuitekeleza katiba. Jamhuri dei njema.

No comments:

Post a Comment