Thursday, December 2, 2010

Kesi yanukia HAGUE...siasa kando, asema Occampo

Washukiwa sita waliopanga ghasia za baada ya uchaguzi watafika mbele ya mahakama ya kimataifa ICC mapema kwaka ujao. Kiongozi mkuu wa mashtaka katika mahakama hiyo Louis Moreno Ocampo amethibitisha kwamba atawaomba majaji wa mahakama hiyo kutoa arifa za sita hao kufika mahakamani kabla ya tarehe 17 mwezi huu. Ocampo aliliambia kongamano la siku mbili la kujadili mabadiliko hapa nchini kwamba washukiwa hao huenda wasishtakiwe hadi mwaka 2012 ama mapema mwaka 2013 kutokana na utaratibu mrefu wa mahakama.  Occampo ameongeza kwamba mahakama hiyo imepata ushahidi mpya kuhusu ghasia hizo na haitategemea ripoti za mashirika ya haki na ile ya Waki. Ocampo pia amewakana mashahidi ambao walikuwa wamedai kwamba walifundishwa jinsi ya kuwashirikisha baadhi ya wanasiasa katika ghasia hizo.

No comments:

Post a Comment