WIZARA YA ELIMU IMEZINDUA RASMI JOPO KAZI LA KUANGANZIA NA KURATIBU MABADILIKO KATIKA SEKTA YA ELIMU KUAMBATANA NA KATIBA MPYA. NA KAMA ANAVYOARIFU NEWTON MUDAKI, JOPOKAZI HILO LINA MUDA WA MIEZI SITA KUKAMILISHA JUKUMU HILO KABLA YA KUWASILISHA MAPENDEKEZO YAKE BUNGENI ILI KUIDHINISHWA.
AKIZINDUA RASMI JOPO KAZI HILO, WAZIRI WA ELIMU PROF SAM ONGERI AMESEMA IPO HAJA YA KURATIBU MABADILIKO YA KINA KATIKA SEKTA HIYO KUHAKIKISHA UGAVI SAWA WA RASLIMALI NA VILE VILE KUIMARISHA VIWANGO VYA ELIMU NCHINI. AIDHA JOPO HILO LINATARAJIWA KUFANYA UCHUNGUNZI KATIKA SEKTA HIYO KUTATHMINI UDHAIFU NA UWEZO WAKE.WAKATI HUO HUO WAZIRI ONGERI AMEWATAHADHARISHA WAKUU WA SHULE DHIDI YA KUWALAZIMISHA WANAFUNZI KURUDIA MADARASA. AMEWATAKA KUTUMIA MBINU MBADALA KUTOA MAFUNZO KWA WANAFUNZI WANAOPITIA WAKATI MGUMU SHULENI.
AIDHA WAZIRI ONGERI AMETETEA MPANGO WA SERIKALI KUZIPANDISHA HADHI SHULE ZA UPILI ZA MIKOA HADI KUWA ZA KITAIFA KATIKA KAUNTI ZOTE. ONGERI AMEPUZILIA MBALI TETESI ZINAZOTOLEWA NA WATAALAM WA MASUALA YA ELIMU KUWA HUENDA HATUA HIYO IKAATHIRI VIWANGO VYA ELIMU NCHINI NA KUSEMA KUWA WANALENGA KUONGEZA IDADI YA WANAFUNZI WANAOJIUNGA NA SHULE ZA UPILI.KULINGANA NA ONGERI KUPANDISHWA HADHI SHULE HIZO NI NJIA MOJA YA KUHAKIKISHA KATIBA INATEKELEZWA KWA KUANGAZIA USAWA KWA WOTE WAKATI WA KUGAWA RASLIMALI ZA KITAIFA.
No comments:
Post a Comment