Wavuvi wakenya wanaohudumu katika kisiwa chenye utata cha Migingo sasa wanailaumu serekali kwa kupuuza kilio chao licha ya masaibu wanayopitia mikononi mwa maafisa wa kiusalama kutoka nchi Jirani ya Uganda waliopiga kambi kisiwani humo.
Wavuvi hao wanalalama kuwa, inakera kuona kuwa licha ya vilio vyao, na dhulma wanazopitia, serikali ya Kenya kupitia wizara husika imesalia kuwa kimya, hali wanayodai kuwa inawapelekea maafisa hao wa kiusalama kuwatesa hata zaidi.
Mwenyekiti wa muungano wa wavuvi wakenya katika Kisiwa hicho, Bw Juma Ombori anadai kuwa maafisa hao wa kiusalama wanaendelea kuwatoza ushuru, kuwanyang’any avifaa vya uvuvi na kuwatia mbaroni wakenya pasi na sababu, hali ambayo sasa imewalazimu baadhi ya wavuvi kuhamia maeneo mengine ili kuendeleza biashara za uvuvi.
Mwenyekiti huyo kwa mara nyingine tena ameiomba serikali haswa vigogo wakuu waziri mkuu Raila Odinga, kuingilia kati suala hilo, huku akidai kuwa wanapotafuta msaada kwa maafisa wilayani na Mikoani, maafisa hao hudai kuwa hilo ni suala la kimataifa linalopaswa kujadiliwa na marais wa mataifa husika
No comments:
Post a Comment