Thursday, January 13, 2011

Tahadhari......Matapeli wanaojifanya maafisa wa jeshi

Wizara ya ulinzi sasaimetoa tahadhari kwa umma dhidi ya genge moja la matapeli, ambalo limekuwa likiwatoza wananchi pesa kwa ahadi za nafasi za kazi ya jeshi. Kundi hilo limekuwa likidai wana uhusiano wa karibu na maafisa wa ngazi za juu katika idara ya ulinzi.

Jamaa hao wamekuwa wakitumia Mpesa zilizo na majina ya maafisa hao wa kijeshi hususan kuwahadaa wananchi kwa vile unapotuma pesa, majina ya maafisa wa kijeshi ndiyo hujiandiklisha, na hivyo kutoa dhana kwa mwananchi asiye na fahamu kuwa pesa zake zimefikia maafisa hao wa kijeshi.

wizara ya ulinzi hivyo inawatahadharisha wakenya kutohadaiwa na mtandao huu wa matapeli,kwa vile nafasi za kazi katika idara ya jeshi hutangazwa wazi magazetini.

No comments:

Post a Comment