Saturday, December 17, 2011
Siasa za tume ya maadili na ufisadi
Nimekuwa nikifuatilia mjadala kuhusu uteuzi wa waliopendekezwa kuhudumu katika bodi ya tume mpya ya maadili na ufisadi.Tayari majina ya walioteuliwa na rais Mwai kibaki na waziri mkuu Raila Odinga yamekataliwa na kamati ya bunge kuhusu sheria na haki. Kamati hii hata hivyio haijatoa sababu maalum za kuwakatalia mbali walioteuliwa. Ningependa kuwaunga mkono wabunge waliopuzilia mbali ripoti ya kamati hiyo ambayo ilisema licha kuwa watatu waliopendekezwa wamehitimu, hawana ile ari ya kukabiliana na ufisadi. Je, ni lini mtu akatuma maobmi ya kazi kama hana ile ari ya kufanya kazi hiyo? Na je, ni lini uwezo wa mtu ukapimwa kwa kumuangalia tu? hivi ndivyo tulivyokosea wakati wa kumteua aliyekuwa mkrurugenzi wa tume ya awali ya kupambana na ufisadi KACC, dkt PLO Lumumba, tulimwamini kutokana na maneno yake na matumizi ya misamiati, kumbe tungalijua! Kazi hakuitekeleza vilivyo, wabunge ni wao wao tu waliomtema nje tena. Hivi nasema kama bunge, wametunukiwa ile uwezo wa kuwapiga msasa na kuwateua watu wanaofaa kuongonza, hatungetarajia kushuhudia migawanyiko kama hii, mjadala kuu ukiwa ni kuhusu ari ya mtu kufanya kazi. nakubaliana na mbunge Wavinya Ndeti, wakati tukimchagua rais Kibaki, alionekana kama mtu asiye na uwezo wa kuongonza, lakini takriban miaka 10 matunda ya uongozi wake ni wazi. Tuwape watatu hawa nafasi ya kuhudumu katika tume hiyo, na itatuchukua muda mchache tu kutambua uweledi wao katika masuala ya kukabiliana na ufisadi. Wahenga walisema usimuone fisi ametulia, anatunga sheria!.. Ni hayo tu wakuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment