Monday, March 14, 2011

Hivi ckujua naweza tishwa

Mkali wao ni kawa nimekaa katika chumba cha habari, nashughulikia kuona habari za mchana saa saba zimefika hewani lakini dah! lizard ajaka pita.......nilijua kwamba pia mimi ni mwoga......usipime!!! usiku mwema lakini

Saturday, March 12, 2011

Kivumbi ni leo

FA CUP LIVE: Manchester United v Arsenal - follow the action from Old Trafford as it happens soma hapa


Monday, March 7, 2011

ku blogu kweli kazi

Am trying to "collect" my mind...kazi ya uhariri sio mchezo,wakati mwingine nakosa nafasi ya kublogu. Walakini tuko pamoja watu wamsangu!!!!

day poaz wakubwa.

Saturday, March 5, 2011

MIGINGO......KILIO CHA WAVUVI WA KENYA

Wavuvi wakenya wanaohudumu katika kisiwa chenye utata cha Migingo sasa wanailaumu serekali kwa kupuuza kilio chao licha ya masaibu wanayopitia mikononi mwa maafisa wa kiusalama kutoka nchi Jirani ya Uganda waliopiga kambi kisiwani humo.

Wavuvi hao wanalalama kuwa, inakera kuona  kuwa licha ya vilio vyao, na dhulma wanazopitia, serikali ya Kenya kupitia wizara husika imesalia kuwa kimya, hali wanayodai kuwa inawapelekea maafisa hao wa kiusalama kuwatesa hata zaidi.

Mwenyekiti wa muungano wa wavuvi wakenya katika Kisiwa hicho, Bw Juma Ombori anadai kuwa maafisa hao wa kiusalama wanaendelea kuwatoza ushuru, kuwanyang’any avifaa vya uvuvi na kuwatia mbaroni wakenya pasi na sababu, hali ambayo sasa imewalazimu baadhi ya wavuvi kuhamia maeneo mengine ili kuendeleza biashara za uvuvi.

Mwenyekiti huyo kwa mara nyingine tena ameiomba serikali haswa vigogo wakuu waziri mkuu Raila Odinga, kuingilia kati suala hilo, huku akidai kuwa wanapotafuta msaada kwa maafisa wilayani na Mikoani, maafisa hao hudai kuwa hilo ni suala la kimataifa linalopaswa kujadiliwa na marais wa mataifa husika